Lyrics: Wapo - Lameck Ditto

"Wapo" from the album "Wapo"
By Lameck Ditto

Siwezi kuishi bila upendo wako ulivyoniteka
Naomba nihifadhi kwa mikono yako nisije anguka
Nimezunguka kutwa nzima kama wewe sijamuona
Napigwa vita chungu nzima lakini bado napigana

Wapo walotaka nikuache nakusema sitofika popote
Ndipo wakanifanya niongeze juhudi nyingi mpaka siku niwe wako
Sijali umenitesa mara ngapi ama nimelia mara ngapi
Nia yangu ni moja siku moja tuwe wote pamoja
Nia yangu ni moja siku moja tuwe wote pamoja

Sijasahau usiku wa manane ule ulivyo nikana
Mbele ya nduguzo na bwanaako yule ukanitukana
Kwa mapenzi nilisimama kama chizi nilionekana
Leo wakusema hakuna najua waamini nakupenda

Wapo walotaka nikuache nakusema sitofika popote
Ndipo wakanifanya niongeze juhudi nyingi mpaka siku niwe wako
Sijali umenitesa mara ngapi ama nimelia mara ngapi
Nia yangu ni moja siku moja tuwe wote pamoja
Nia yangu ni moja siku moja tuwe wote pamoja

Penzi letu liende mbele lisifike mwisho oooooo
Tuwe wote milele tushinde vikwazo oooooo
Wapooooo ooo oooo oo wapooooooooooo
Wapoooooooo wapooooooooooooooo

Sijali umenitesa mara ngapi ama nimelia mara ngapi
Nia yangu ni moja siku moja tuwe pamoja haaaaaa
Nia yangu ni moja siku moja tuwe pamoja haaaaaa

Lyrics: Wapo - Lameck DittoSocialTwist Tell-a-Friend

No comments:

Post a Comment

Submit your comments here: