Lyrics: Karubandika - Orchestra Maquis Original

"Karubandika" from the album "Karubandika"
By Orchestra Maquis Original

Kama wewe ungenipenda
Kwa nini kunidanganya bwana wee
Kujibandika madaraka sio yako bwana wewe

Nimesikia tetesi kuwa huna lolote hata kazi huna eeh
Unazurura mchana kutwa eeh
Kupita kurandaranda mitaani

Kumbe hukuwa na uwezo wa kunioa ila kuniharibia maisha
Heri kuniambia, ukweli ulivyo kuliko kunidanganya

Nikuelewe vipi eh
Babu eh
Uaminifu wako uko wapi eh
Papa

Usinione pweke baba
Usinione pweke baba

Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh
Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh

Haya yote ni matatizo ya dunia baba
Haya yote ni matatizo ya dunia baba

Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto mie
Kumbe bwana yule
Hana kitanda wala shuka
Pa kulala hana
Analala kwenye stendi ya basi
Pa kulala hana
Anakesha kwenye kituo cha punda
Karubandika yoyo
Acha vituko wee baba

Usinione pweke baba
Usinione pweke baba

Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh
Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh

Haya yote ni matatizo ya dunia baba
Haya yote ni matatizo ya dunia baba

Akiingia kwenye baa
Kazi yake kuomba bia
Akiingia kwenye baa
Kazi yake kuomba bia

Hana hata aibu eh
Sigara pia anaomba
Mitaani na kwenye mastovu
Hujitangazia kuwa yeye
Ni mkurugenzi wa kampuni fulani oh
Kumbe sivyo hivyo

Usinione pweke baba
Usinione pweke baba

Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh
Kwa kukubali wito wako
Karubandika eh

Haya yote ni matatizo ya dunia baba
Haya yote ni matatizo ya dunia baba


Review
MP3



Lyrics: Karubandika - Orchestra Maquis OriginalSocialTwist Tell-a-Friend

5 comments:

Submit your comments here: