Lyrics: Amua Nikuachie Kazi – Maroon Commandos

“Amua Nikuachie Kazi” from the album “Swahili Special Hit Parade 1983”

Eeh bwana
Nashindwa na mambo yako
Na nyumbani hata kidogo hutoki eeh

Hata shughuli za nyumba hazifanyiki
Kwani saa zote bwana huko nyumbani

Mara kwa mara wee waingia jikoni bwana
Naona nikuwachie upishi

Ewe bwana badili tabia
Uwe kama wenzako

Tangu lini wapishi wawili wapike chungu kimoja
Tangu lini wapishi wawili wapikie chungu kimoja

Amua mwenyewe
Nikuwachie kazi

Kubishana na wee pamoja na watoto kumenichosha
Kubishana na wee pamoja na watoto kumenichosha

Onja onja chakula
Kwa sufuria sio vyema

MP3 Download Links! Click on your favorite song.
Lyrics: Amua Nikuachie Kazi – Maroon CommandosSocialTwist Tell-a-Friend

No comments:

Post a Comment

Submit your comments here: